MAREFA WA UGANDA KUCHEZESHA TANZANIA NA MADAGASCAR

4 miezi iliyopita 209
ARTICLE AD BOX

REFA Ssali Mashood atapuliza kipyenga kwenye mechi ya Kundi J kufuzu Kombe la Dunia Jumanne baina ya wenyeji, Tanzania na Madagascar Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Ssali atasaidiwa na Waganda wenzake, Okello Dick na Katenya Ronald watakaokuwa wanakimbia vibendera pembezoni mwa Uwanja, wakati Subilla Ali Chelangat atakuwa mezani.
Mtathmini wa mchezo huo anatarajiwa kuwa Ahmed Ali Mohamed wa Somalia na Kamisaa ni Shilunga Erastus wa Namibia.


Soma chapisho lote